Ndemla ashindwe mwenyewe kwa Vanderbroeck

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Dec 2019
Ndemla ashindwe mwenyewe kwa Vanderbroeck

Wakati wa Said Ndemla kutambulika rasmi kama mfalme wa klabu ya Simba umewadia, hasa baada ya ujio wa kocha mpya, Sven Ludwig Vanderbroeck ambaye ameonyesha kukunwa na kipaji alichonacho kiungo huyo.

Inafahamika wazi kuwa Ndemla ni mhanga wa ufinyu wa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Wekundu wa Msimbazi kutokana na utitiri wa viungo walio na uwezo mzuri, wakiwamo Jonas Mkude na Mzamiru Yassin.

Wengine ambao wanacheza nafasi sawa na Ndemla katika kikosi cha Simba ni Gerson Fraga, Francis Kahata, Clatous Chama, Sharaf Eldin Shiboub na hata Ibrahim Ajib.

Lakini juhudi ambazo Ndemla amezionyesha ndani ya muda mfupi wa kufanya kazi na kocha wake mpya, Vandenbroeck na ukichanganya na kipaji chake kikubwa, vimetosha kumpa Mbelgiji huyo tabasamu la kuwa na mchezaji wa aina yake.

Sifa kubwa ya Ndemla tangu alipoanza kuitumikia timu ya wakubwa ya Simba ni uwezo wake wa kupiga mashuti ya mbali yanayoweza kuzaa mabao kitu ambacho asilimia kubwa ya viungo wa timu hiyo wanakikosa.

Na hilo ni miongoni tu mwa vitu ambavyo Vandenbroeck amekuwa akionekana kuvisisitiza kwa Ndemla kuhakikisha anavifanya kwa ufanisi. Vingine vikiwa ni kumiliki mpira, kupiga pasi za uhakika na kutoa asisti zinazoweza kuzaa mabao.

Hata hivyo, kocha huyo ameonekana kumuhitaji zaidi Ndemla kuufanyia kazi ubora wa mashuti yake ili aweze kufunga mabao pale inapotokea nafasi ya kufanya hivyo kutokana na kwamba ni kitu kinachompiga chenga kiungo huyo.

Iwapo Ndemla atafanya kile ambacho kocha huyo anakitaka kutoka kwake ni wazi atakuwa ndiye mfalme katika himaya ya Simba msimu huu sambamba na kupewa nafasi ya kutosha ya kucheza tofauti na utawala wa makocha waliopita.

Katika mazoezi ya Simba yanayofanyika katika Uwanja wa MO Simba Arena, Vandenbroeck mara kwa mara ameonekana kuzungumza na Ndemla na muda mwingine akimtuma Seleman Matola kumuelekeza vitu vya kufanya kiungo huyo.

Hii ina maana kuwa kocha huyo amegundua Ndemla ana kitu cha ziada ambacho kinaweza kuja kumsaidia katika kikosi atakachokipanga kwa ajili ya mechi zilizopo mbele yao msimu huu.

Iwapo Ndemla ataweza kutimiza yale anayotakiwa kufanya na kocha wake huyo ni wazi atakuwa tishio kubwa kwa wenzake ambao tayari wameshajihakikishia kudumu kwenye kikosi cha kwanza tangu wakiwa chini ya kocha Aussems

Bingwa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’