Kili Stars yatoka 'patupu' Uganda

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Dec 2019
Kili Stars yatoka 'patupu' Uganda

Mabao mawili ya Kenneth Muguna na Abdallah Hassan yameifanya timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' kutoka mikono mitupu katika mashindano ya Chalenji baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Kenya katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu

Katika mchezo huo ulioanza saa 7:00 mchana, Kenya walitumia vyema makosa binafsi ya wachezaji wa Stars, kuweza kupachika mabao hayo ambayo yameifanya Kenya imalize kipindi cha kwanza ikiwa inaongoza kwa mabao 2-0 huku bao la kufutia machozi la Kilimanjaro Stars likifungwa kipindi cha pili na Gadiel Michael.

Ikionekana kama inacheza kukamilisha ratiba, Kilimanjaro Stars imeonekana kushindwa kuchangamka na kundi kubwa la wachezaji wake linaonekana kucheza ili mradi tu, hali ambayo imetumiwa vyema na Kenya kuwaadhibu.

Kenya ambao walionekana kucheza kwa hesabu zaidi, walikuwa wepesi katika kuanzisha mpira kila wanapoupokonya kutoka kwa wachezaji wa Kilimanjaro Stars na kushambulia kwa haraka jambo ambalo limeonekana kuzaa matunda kwa upande wao.

Dakika ya 16 tu ya mchezo, Muguna aliwainua vitini Kenya baada ya kuwapachikia bao la kuongoza akiunganisha kwa shuti la wastani, pasi ya Oscar Wamalwa.

Kabla ya kupiga pasi hiyo, Wamalwa alimzidi ujanja Kelvin Yondani ambaye alishindwa kumkaba na kumpiga chenga kisha kuupeleka mpira huo kwa Muguna ambaye hakufanya ajizi kuujaza wavuni.

Dakika 12 baadaye, Kenya nusura waandike bao la pili lakini kiungo wake Lawrence Juma akiwa analitazama lango baada ya kupokea pasi ya Moses Mudavadi, alipiga shuti lililotoka nje.

Stars haikuonekana kujifunza kutokana na bao la kwanza na badala yake ikaendelea kurudia makosa yaleyale ya kupiga pasi ambazo hazikufikia walengwa lakini pia kupoteza mipira mara kwa mara.

Uzembe wa kiungo Mzamiru Yassin kuchelewa kuachia mpira kwa haraka pindi Kilimanjaro Stars ilipokuwa inaumiliki, uliigharimu timu kwa kuwa chanzo cha Kenya kufunga bao la pili.

Wakati idadi kubwa ya wachezaji ikiwa imeuvuka mstari unaogawa uwanja na kuwa kwenye nusu ya Kenya, Mzamiru ambaye alichelewa kutoa pasi, alijikuta akiporwa mpira na Antony Wambani ambaye alimpasia kwa haraka Hassan aliyeimalizia kiustadi kwa staili ya kubetua na kuujaza wavuni.

Baada ya kuingia bao hilo, Stars ilijaribu kujitutumua na kulazimisha kupenya safu ya ulinzi ya Kenya lakini ilikosa ubunifu na kupelekea ipoteze mipira mingi ya mwisho jirani na lango la Kenya.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
13h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
13h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
16h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’