Mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula amepata majeraha yaliyomfanya ashindwe kumaliza mchezo wa nusu fainali michuano ya Chalenji kati ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Uganda Cranes
Mchezo huo uliopigwa uwanja wa KCCA, uliishuhudia Uganda ikitinga fainali baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Manula alipata majeraha kwa kugongana na mchezaji wa Uganda wakati mchezo ukielekea mapumziko
Majeraha hayo huenda yakamuweka nje kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Arusha Fc ambao utapigwa Jumapili Disemba 22 kwenye uwanja wa Uhuru

ADVERTISE HERE