Nitarejesha makali yangu - Niyonzima

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
5 Jan 2018
Nitarejesha makali yangu - Niyonzima
Kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima, amewataka mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na hofu na uwezo wake na atarudi kwenye kiwango chake baada ya kupona majeraha ya kifundo cha mguu yanayomkabili.

Niyonzima yupo nje ya uwanja akiuguza majeraha hayo na ameachwa kwenye kikosi cha timu hiyo kinachoshiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.

Katika mahojiano na gazeti la Nipashe, Niyonzima, amesema anaumia kukaa nje na kushindwa kuitumikia timu yake, lakini hana namna lazima ahakikishe amepona majeraha yake.

“Mashabiki wanivumilie nipone, nitarejea uwanjani hivi karibuni, kwa kweli ninaumia kuwa nje, lakini sina namna,” alisema Niyonzoma.

Alisema kwa sasa anaendelea vizuri na atajiunga na wenzake kwenye maandalizi ya michezo ya Ligi Kuu.Kocha Masoud Djuma, amemwacha Niyonzima kwenye kikosi cha Simba alichoenda nacho Zanzibar, ili kumpa fursa ya kupona kabisa majeraha yake.

Simba inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, juzi ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Mwenge FC ya Pemba kwenye mechi ya ufunguzi ya Kombe la Mapinduzi. Jana ikaichapa Jamhuri mabao 3-1.

Ikimaliza michuano hiyo ina kibarua kigumu cha mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Singida United.

Katika michuano hiyo Simba ipo Kundi A pamoja na URA, Jamhuri, Mwenge na Azam FC, wakati watani zao, Yanga wakiwa Kundi B ambalo linajumuisha timu ya Zimamoto, Mlandege, JKU, Taifa Jang’ombena Singida United.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
57m ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE →
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
18h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
20h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
22h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE →