Kwasi alivyoweka rekodi Zanzibar

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Jan 2018
Kwasi alivyoweka rekodi Zanzibar
Baol alilofunga beki wa Simba Asante Kwasi dhidi ya Jamhuri limeingia kwenye rekodi kadhaa.

Beki huyo ambaye usajili wake kutoka Lipuli kwenda Simba ulipamba headlines za michezo Bongo amefunga goli lake la kwanza akiitumikia Simba kwa mara ya kwanza ikiwa ni mechi yake ya kwanza ya Mapinduzi Cup lakini akicheza kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.

Mtangazaji wa Azam TV Pascal Kabombe wakati akitangaza goli hilo alisikika akisema: Ò€œAsante Kwasi amefunga goli lake la kwanza akiichezea Simba kwa mara ya kwanza lakini ni mara yake ya kwanza kucheza kwenye uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.Ò€

Goli hilo lilikuwa ni la tatu kwa Simba katika mchezo huo baada ya John Bocco na Moses Kitandu kutangulia kufunga magoli mawili ya mapema.

Simba imefikisha pointi nne baada ya kucheza mechi mbili, mchezo wa kwanza walilazimishwa sare ya kufungana goli 1-1 na Mwenge.

Pointi nne zinawafanya wapande hadi nafasi ya pili nyuma ya Azam ambao wana pointi sita wakiwa wamecheza mechi mbili pia.

Kwasi ndio mambo yake kufunga, akiwa na Lipuli tayari alishafunga magoli matano kwenye ligi kuu ya Tanzania bara akiwa ndiye beki mwenye magoli mengi zaidi hadi sasa.

Magoli hayo (matano) yanamfanya kuwa nyuma kwa magoli matatu dhidi ya mchezaji anaeongoza kwa magoli hadi sasa ambaye ni Emanuel Okwi.

Kwa hisani ya ShaffihDauda
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
38m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’