Kiungo wa Polisi Tanzania Baraka Majorogo huenda ukawa usajili wa kwanza wa Simba dirisha dogo
Dirisha dogo la usajili litafunguliwa kesho Jumatatu Disemba 16 ambapo timu za ligi kuu na ligi daraja la kwanza zitakuwa na nafasi ya kuimarisha vikosi vyao
Mabingwa watetezi Simba hawatarajiwi kuwa na maboresho makubwa kwani kikosi chao mpaka sasa kimeonekana kuwa imara
Majogoro anahusishwa kujiunga na mabingwa hao wa nchi yakiwa ni mapendekezo ya kocha msaidizi, Selemani Matola
Kiwango alichoonyesha timu ya Polisi Tanzania, kimempa nafasi ya kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' ambacho jana kilitinga nusu fainali ya michuano hiyo inayofanyika nchini Uganda
Maboresho mengine huenda yakafanywa kwenye safu ya ushambuliaji