Uzinduzi wa kadi za mashabiki Simba ni kesho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Dec 2019
Uzinduzi wa kadi za mashabiki Simba ni kesho

Hafla ya uzinduzi wa kadi za mashabiki wa klabu ya Simba utafanyika kesho Jumamosi, Disemba 14 viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam

Tukio hilo la kihistoria linatarajiwa kuanza saa mbili kamili asubuhi

Mashabiki wa klabu ya Simba wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo bila ya kusahau kubeba kitambulisho cha Taifa (au namba) au kitambulisho cha mpiga kura ili waweze kujipatia kadi ya shabiki

Gharama ya kadi ni Tsh 22,000/- tu na itakuwa na faida hizi;

MWANACHAMA WA SIMBA

1. Ana Haki ya kuwa mpiga kura katika chaguzi mbalimbali ndani ya Club.
2. Ana haki ya Kugombea au kuchagua/Kuchaguliwa nafasi mbalimbali ndani ya Club.
3. Ana haki ya Kuhudhuria mkutano yote rasmi eneo lake ikiwemo Mkutano Mkuu wa Club.
4. Aha haki ya kutoa ya maamuzi ya Mkutano Mkuu.
5. Ni mmiliki wa hisa ndani ya Club.
6. Faida za E-card zote anapata.

MSHABIKI WA SIMBA

1. Ana Haki ya muda ya kuchagua, kuchaguliwa katika eneo lake lenye usajili/utambuzi wa muda tu.
2. Ana haki kutambuliwa rasmi na club kama muombaji mpya uanachama.
3. Faida za E-card zote anapata.

FAIDA ZA E-CARD

1. Kuwa na matumizi yote ya kama zingine za ATM.
2. Kuwa na mfumo wa kutambuliwa rasmi na kuwekwa kwenye Database ya Club.
3. Kuweza kutoa au kuweka fedha kwenye Account yako popote ulipo sio mpaka uende Bank (online system).
4. Unaweza kununua bidhaa mbalimbali popote penye machine ya Equity bank.
5. Kulipia Ada yako ndani ya Club automatically.
6. Kununua Bidhaa za Simba na zenye punguzo lenye faida kwa mawakala wetu.
7. Kuweza kuingilia Uwanjani kwa taratibu zinazoendelea kuwekwa katika mfumo.
8. Kuweza kutambuliwa popote kwa mfumo wa Digital kama wewe ni Mwana Simba.
9. Kusaidia Club kupata mapato na kuzuia upotevu wa fedha

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’