Malizeni migogoro hatutaki visingizio Januari 04 - Kaduguda

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Dec 2019
Malizeni migogoro hatutaki visingizio Januari 04 - Kaduguda

 Wakati tambo za watani wa jadi zikiwa zimeanza kushika kasi, Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda, amewatahadharisha Yanga kujipanga kuelekea mechi hiyo.

Simba itakutana na Yanga mwakani Januari 4 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mechi ambayo inatarajiwa kuwa ya aina yake.

Kaduguda amewapa tahadhari Yanga kwa kuwaambia wamalize migogoro yao mapema ili waepuke kukutana na kichapo cha maana.

Amewaomba wawe na tahadhari kwani wao wanazidi kujipanga na akiwaomba endapo wakifungwa wasije kusema sababu tulikuwa na migogoro.

"Tunawaomba wenzetu wajiandae vizuri kwani sisi tuko katika maandalizi.

"Vema wakamaliza migogoro yao haraka ili baadaye wasije leta visingizio kuwa wamepoteza kwa kuwa hawako vizuri," alisema

Simba tayari imerejea mazoezini kujiwinda na mchezo huo pamoja na michezo mingine

Leo Kocha Mkuu wa timu hiyo Sven van Der Broeck ataongoza mazoezi uwanja Mo Simba Arena

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12m ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
15h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
15h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
18h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’