Vandenbroeck ni kocha anayetafuta mafanikio kama ilivyo kwa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Dec 2019
Vandenbroeck ni kocha anayetafuta mafanikio kama ilivyo kwa Simba

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ambaye alitambulishwa jana, alianza kuwa kocha mkuu katika timu ya Niki Volou, iliyopo nchini Ugiriki mwaka 2014, akiwa kama kocha wa muda (Caretaker).

Baada ya hapo akawa kocha msaidizi wa timu ya Oud-Heverlee Leuven na timu ya taifa ya Cameroon, ambayo alikuwa akifanya kazi ya usaidizi chini ya kocha mkuu Hugo Broos, ambapo mwaka 2017, walichukua ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika.

Vandenbroeck, baada ya hapo alikwenda kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zambia Julai 2018, baada ya kuingoza timu hiyo Februari 2019, Shirikisho la soka la Zambia, walitangaza kutokuongeza mkataba wa kocha huyo aliokuwa na timu hiyo kwa mwaka mmoja.

Zambia waliamua kuvunja mkataba wa Vandenbroeck, Machi 2019, kutokana na kushindwa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika zilizofanyika nchini Misri.

Sven Ludwig Vandenbroeck, amezaliwa Septemba 22, mwaka 1979, mpaka sasa ametimiza miaka 40, amezaliwa katika Mji wa Vilvoorde, nchini Belgium.

Kabla ya kuwa kocha alianza kucheza mpira kama kiungo mkabaji mwaka 1996–2000, katika timu ya Mechelen, baada ya hapo mwaka 2000–04, alikwenda kujiunga na timu ya Roda JC ambapo alicheza mechi 55

Mwaka 2004–05, Vandenbroeck alijiunga na De Graafschap ambapo napo alicheza mechi 19, kisha baadae kujiunga na timu ya Akratitos mwaka 2005

Vandenbroeck mwaka 2006–07, alijiunga na Lierse ambapo napo alicheza mechi 23 na mwaka 2007–08, alijiunga na Vise na baada ya msimu kumalizika mwaka 2009, alijiunga na Lov-Ham ambapo alicheza michezo mitatu

Uongozi wa klabu ya Simba umemchukua kocha huyo baada ya kuridhishwa na mipango na kiu yake ya mafanikio kama kocha

Simba ina muelekeo huo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
12h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’