Uzinduzi wa kadi za Mashabiki wa klabu ya Simba utafanyika Disemba 14 viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam
Fahamu faida ambazo Mwanasimba unaweza kupata ukiwa na kadi hii;
MWANACHAMA WA SIMBA
1. Ana Haki ya kuwa mpiga kura katika chaguzi mbalimbali ndani ya Club.
2. Ana haki ya Kugombea au kuchagua/Kuchaguliwa nafasi mbalimbali ndani ya Club.
3. Ana haki ya Kuhudhuria mkutano yote rasmi eneo lake ikiwemo Mkutano Mkuu wa Club.
4. Aha haki ya kutoa ya maamuzi ya Mkutano Mkuu.
5. Ni mmiliki wa hisa ndani ya Club.
6. Faida za E-card zote anapata.
MSHABIKI WA SIMBA
1. Ana Haki ya muda ya kuchagua, kuchaguliwa katika eneo lake lenye usajili/utambuzi wa muda tu.
2. Ana haki kutambuliwa rasmi na club kama muombaji mpya uanachama.
3. Faida za E-card zote anapata.
FAIDA ZA E-CARD
1. Kuwa na matumizi yote ya kama zingine za ATM.
2. Kuwa na mfumo wa kutambuliwa rasmi na kuwekwa kwenye Database ya Club.
3. Kuweza kutoa au kuweka fedha kwenye Account yako popote ulipo sio mpaka uende Bank (online system).
4. Unaweza kununua bidhaa mbalimbali popote penye machine ya Equity bank.
5. Kulipia Ada yako ndani ya Club automatically.
6. Kununua Bidhaa za Simba na zenye punguzo lenye faida kwa mawakala wetu.
7. Kuweza kuingilia Uwanjani kwa taratibu zinazoendelea kuwekwa katika mfumo.
8. Kuweza kutambuliwa popote kwa mfumo wa Digital kama wewe ni Mwana Simba.
9. Kusaidia Club kupata mapato na kuzuia upotevu wa fedha.
10. Account yako fedha unazoweka hazikatwi makato yeyote yale mpaka utapoteza kuzitumia au kuzitoa ndio gharama zinatozwa na hapohapo Simba inapata 50% yake. MxFANO: kununua Luku kwanini ukinunua kupitia card kwa gharama zilezile ila badala ya kile unachokatwa kwenda kwenye mitandao mingine sasa kinakwenda pia na Simba. *UFAFANUZI:*
Kwa wote wenye Account sasa Za Equity Bank ili waweza kuwa na Simba Card au Simba Account ni lazima wafanye au wakubali moja kati ya yafuatayo;
1. Kufungua Account mpya ya Simba Account na kumiliki acc mbili tofauti.
2. Kufunga Account ya sasa na kubadili kuwa ya Simba Account pale unapenda kufungua taratibu zinafanyika kuhulishwa kwa Data tu.
Tunazindua rasmi Kwenye viwanja vya Sabasaba Jumamosi hii ya tarehe 14,, muhimu kuja na kitambulisho cha Taifa na kadi itatolewa kwa shilingi 22,000 tu