Beki Asante Kwasi jana alifunga moja ya mabao ya Simba katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Jamhuri.
Baada ya kutoka sare katika mchezo wake wa kwanza kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar, Simba imerejesha matumaini yake ya kusonga mbele baada ya ushindi huo ulioiwezesha kufikisha alama nne na kushika nafasi ya pili nyuma ya Azam FC yenye alama sita.
Nahodha John Bocco na kinda Mosses Kitandu walifunga mabao mengine ya Simba katika mchezo ambao Simba ilitawala kwa muda mwingi.
Kaimu kocha wa Simba Masudi Djuma alifanya mabadiliko ya kikosi kilichotumika katika mchezo wa kwanza kwa kuwajumuisha Kwasi, Gyan na Kazimoto kwenye kikosi cha kwanza.

ADVERTISE HERE