Michuano ya Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo mitatu kufanyika Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar, vigogo Simba na Yanga wakirejea kazini.
Mchezo utakaotangulia utakuwa wa kiporo kati ya Taifa Jan'gombe na Singida United mapema Saa 8:30 mchana.
Mechi hiyo ililazimika kuahirishwa jana baada ya dakika 45 tu za kipindi cha kwanza kufuatia mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha Uwanja wa Amaan kujaa maji. Na ilivunjika Singida United wakiwa wanaongoza kwa mabao 3-1.
Baada ya mchezo huo, mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC watakutana na timu ngumu ya JKU Saa 10:30 jioni katika mchezo mwingine wa Kundi B.
Simba itakamilisha mechi za leo kwa kumenyana na Jamhuri katika mchezo wa Kundi A Saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan.
Ikumbukwe katika mechi za kwanza juzi, Simba ililazimishwa sare ya 1-1 na Mwenge na Yanga ilishinda 2-1 dhidi ya Mlandege.

ADVERTISE HERE