Djuma kubadili kikosi cha Simba leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Jan 2018
Djuma kubadili kikosi cha Simba leo
Sare ya bao 1-1, dhidi ya Mwenge huenda ikamfanya kaimu kocha mkuu wa klabu ya Simba Masoud Djuma, kufikiria kubadili kikoi chake kwenye mchezo wa leo dhidi ya Jamhuri FC.

Djuma amefunguka kuwa hakutegemea kupata sare katika mchezo huo lakini hana budi kuyakubali matokeo hayo kwasababu mchezo wa soka ndivyo ulivyo wakati mwingine unapata kile ambacho hujakitegemea.

"Tulivyouanza mchezo nilidhani mambo nimepesi lakini baadaye hali iligeuka licha ya kutengeneza nafasi nyingi lakini tulishindwa kuzitumia na siwezi kumlaumu mchezaji yeyote kwasababu hivi nivitu vya kawaida kwenye mchezo wa soka kitu cha msingi ni kujipanga upya ili mchezo unaokuja tuweze kushinda," amesema Djuma.

Kocha huyo amesema mipango yake katika mchezo wa leo ni kubadilisha kikosi kwa kuwatumia wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza kinachocheza ligi badala ya wengi aliowaanzisha juzi dhidi ya Mwenge ambao wamekuwa wakitumika kama wachezaji wa akiba.

"Niliona nibadili kikosi kwa kuwatumia wachezaji wengi wale ambao wamekuwa wakikaa benchi na kuwapumzisha wale ambao wamekuwa wakitumika mara kwa mara kwenye mechi za ligi nashukuru walifanya kazi yao vizuri lakini mechi ijayo nalazimika kubadili kikosi kwasababu tunataka kushinda ili kutimiza malengo ya timu ambayo ni ubingwa," amesema Djuma.

Mrundi huyo amesema kitu kingine ambacho kinamlazimu kubadilisha kikosi mara kwa mara kwenye michuano hiyo ni muda mdogo wa mapumziko ambao hauwapi nafasi wachezaji kupumzika na kujiandaa na mechi nyingi jambo ambalo amewashauri waandaji kuliangalia.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’