Chambeshi atajwa kumrithi Aussems Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Dec 2019
Chambeshi atajwa kumrithi Aussems Simba

Klabu ya Simba inaendelea na mchakato wa kusaka kocha mpya baada ya kumtimua Patrick Aussems wiki iliyopita

Makocha wengi wamehusishwa na nafasi hiyo, ambayo kwa hadhi ya Simba ya sasa, ni heshima kubwa kuwa kocha wa mabingwa hao wa nchi

Jina la Beston Chambeshi raia wa Zambia ni miongoni mwa majina yanayotajwa sana kuwa mbioni kurithi mikoba ya Aussems

Baadhi ya vyombo vya habari nchini Zambia vimeripoti kuwa klabu ya Simba imefanya mazungumzo na kocha huyo ambaye kwa sasa anainoa timu ya Taifa ya Zambia U23

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 pia amewahi kuzinoa timu za Power Dynamo na Nkana Fc

Ndiye aliyekuwa mkufunzi wa kikosi cha Nkana ambacho kiliondoshwa na Simba kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliopita

Chambeshi hupendelea zaidi kutumia mfumo wa 4-2-3-1, ni muumini wa soka la kumiliki mpira na kushambulia kwa kasi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
47m ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
20h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’