Kiungo Polisi Tanzania ahusishwa kutua Simba dirisha dogo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Dec 2019
Kiungo Polisi Tanzania ahusishwa kutua Simba dirisha dogo

Kiungo fundi wa mpira anayekipiga Polisi Tanzania, Baraka Majogoro yupo mbioni kujiunga na Simba kuungana na kocha wake Seleman Matola anayehusishwa kwenda kuwa kocha msaidizi Msimbazi

Imeelezwa kuwa Matola atakapoondoka Polisi anatarajiwa kuambatana na Majogoro

Hata hivyo, ili kumnasa kiungo huyo ni lazima itumike nguvu kubwa ya kuvunjwa kwa mkataba wa mchezaji huyo, kwani bado amebakiza miezi nane ya kuitumikia

Inaelezwa kwa upande wa Simba hautaki kufanya mambo yao kwa presha na jambo lililopo kwa sasa ni kutaka kuvunja mkataba wa mchezaji huyo ifikapo dirisha dogo (Desemba 15)

Makamu Mwenyekiti wa Polisi, Robert Munisi alipoulizwa juu ya taarifa hizo alisema kwa namna wachezaji wao wanavyojituma haishangazi kuona wakihitajika na klabu mbalimbali

Munisi alisema kwa taarifa ya Majogoro kuhitajika Simba kwake ni ngeni, ila hilo haliwezi kuwazuia Simba kumsajili mchezaji huyo kama tu wakifuata taratibu zilizopo kwenye mkataba

"Kwenye mkataba kuna vipengele vya kuingia na pia kuvunja mkataba, kwa hiyo kama Simba wanamtaka Majogoro na wanatakiwa wakaisome hiyo mikataba ndio wajue wanaivunjaje,” alisema

Majogoro alipoulizwa kuhusu kupata dili hilo alisema kuna kiongozi wa Simba (jina kapuni) aliwahi kumpigia simu na kumwambia wanamfuatilia na anatakiwa kuzidi kujituma

"Siwezi kusema lolote kwani bado nina mkataba na Polisi, ngoja tuone itakavyokuwa ikifanikiwa sawa, lakini ni uongozi ndio utakaoamua," alisema nyota huyoa aliyepo pia timu ya taifa.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’