Takwimu alizoacha Aussems Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Dec 2019
Takwimu alizoacha Aussems Simba

Jana Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba ilichukua uamuzi mgumu wa kumfuta kazi aliyekuwa kocha Mkuu Patrick Aussems ambaye amedumu Msimbazi kwa msimu mmoja na miezi kadhaa

Aussems ameiongoza Simba kuanzia msimu uliopita, ambapo mafanikio makubwa aliyopata ni kutetea ubingwa wa ligi kuu pamoja na kutinga hatua ya robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa

Katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara Aussems ameiongoza Simba katika michezo 48, ameshinda mechi 37, ametoka sare mechi saba na kufungwa mechi nne tu

Katika michezo hiyo Simba ilifunga mabao 96, kufungwa mabao 18 ikijikusanyia pointi 118

Ameweka rekodi ya wastani wa ushindi wa asilimia 77 (win rate 77%)

Katika michuano ya ligi ya mabingwa, Aussems aliiongoza Simba kwenye mechi 14, ameshinda sita, amepoteza tano na sare tatu

Katika michuano hiyo Simba imefunga mabao 20, imefungwa mabao 22 ikijikusanyia jumla ya alama 21

Kwa michuano ya ligi ya mabingwa, Aussems ameweka rekodi ya wastani wa ushindi wa asilimia 42 (win rate 42%)

Pia chini yake Simba ilishiriki michuano mingine kama kombe la Mapinduzi (alifika fainali), Ngao ya Jamii (alishinda mara mbili) na kombe la FA (alitolewa raundi ya kwanza)

Kwa ujumla Aussems aliiongoza Simba katika michezo 63, akishinda mechi 43, akifungwa mechi 10 na kutoka sare mechi 10

Wastani wa ushindi ni asilimia 68 (win rate 68%)

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
50m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’