Matola mguu sawa kurejea Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Dec 2019
Matola mguu sawa kurejea Simba

Wakati uongozi wa klabu ya Simba ukiendelea kusaka Kocha Mkuu baada ya kumtimua Patrick Aussems, kocha wa Polisi Tanzania Selemani Matola yuko mbioni kurejea Msimbazi kuwa kocha msaidizi

Inaelezwa jina la Matola limepitishwa baada ya kujiridhisha na uwezo wake lakini wameona ni wakati sahihi kwake kurejea Msimbazi

Matola amekuwa familia ya Simba kwa muda mrefu. Pamoja na kufundisha timu nyingine, Matola amekuwa akishirikishwa katika masuala mbalimbali na uongozi wa Simba

Aliwahi kuwa nahodha na baadae kocha wa timu ya vijana kisha kupandishwa timu ya wakubwa kuwa msaidizi wa Dyran Kerr

Uwezo wake wa kutambua wachezaji wenye vipaji unatajwa kumbeba kupewa majukumu na Simba

Ukitaja nyota kama Ibrahim Ajib, Haruna Shamte, Jonas Mkude, Mohammed Hussein, Miraji Athumani, Ramadhani Singano 'Messi', Said Ndemla, Haruna Chanongo, Humud, Makame na wengine wengi tu walipita mikononi mwa Matola

Matola analifahamu vyema soka la Tanzania, anawafahamu vyema wachezaji wa Kitanzania ndio maana amekuwa akipata maanikio hata akiwa na timu ndogo

Pamoja na kuinoa Polisi Tanzania, Matola ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inayonolewa na Etienne Ndayiragije

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’