Rasmi : Simba yatangaza kumfuta kazi Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Dec 2019
Rasmi : Simba yatangaza kumfuta kazi Aussems

Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake Mkuu Patrick Aussems kuanzia leo Jumamosi, Novemba 30 2019

Taarifa iliyotolewa na Simba imeeleza uamuzi huo umechukuliwa baada ya Aussems kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa viwango na malengo ambayo klabu ya Simba ilikubaliana nae katika mkataba wake

Miongoni mwa makubaliano hayo ni kuifikisha Simba hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Aidha taarifa hiyo imesema Aussems alipewa nafasi ya kujitetea kwenye kikao cha Kamati ya nidhamu ambako alikuwa akikabiliwa na tuhuma za kuondoka kituo cha kazi bila ya ruhusa ya uongozi

Utetezi wake haukutosheleza ikiwa ni pamoja na kukataa kutoa taarifa ya wapi alikokuwa ameenda

Taarifa hiyo imesema mchakato wa kumtafuta Kocha Mkuu umeanza mara moja ambapo kwa sasa kocha Msaidizi Denis Kitambi ameteuliwa kukaimu nafasi hiyo mpaka pale mchakato wa kumpata kocha utakapokamilika

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’