Basi la Coastal Union lahusika ajali ya mashabiki wa Bondia Mwakinyo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Nov 2019
Basi la Coastal Union lahusika ajali ya mashabiki wa Bondia Mwakinyo

Jana ilikuwa siku ya furaha kwa mashabiki wa Bondia Mwanamsimbazi Hassan Mwakinyo ambaye alimpiga kwa pointi mpinzani wake Arnel Tinampay kutoka Ufilipino katika pambano la raundi 10 lililopigwa uwanja wa Uhuru

Hata hivyo imekuwa huzuni kwa baadhi ya mashabiki ambao walisafiri kutoka jijini Tanga kumuunga mkono Mwakinyo baada ya kupata ajali usiku wakati wakirejea Tanga

Ajali hiyo imetokea eneo la Kerege wilayani Bagamoyo, ambapo mashabiki hao waliotumia basi la Coastal Union, lililogongana na lori

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Coastal Union Hafidh Kido imewataja waliofariki kuwa ni Ibrahim Omar na Hussen Saleh ambapo uongozi wa Coastal kwa kushirikiana na ndugu zao, wanafanya taratibu za kuwasafirisha kwenda Tanga kwaajili ya maziko

Hadi sasa miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

"Majeruhi walikuwa wanane, mmoja hali yake ilibadilika amepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na mwingine tumemkuta hapa anaitwa Aziza, ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kwakaheza mkoani Tanga. Abiria wengine tayari wamerejea Tanga wakiwa pamoja na dereva wa gari letu," imeeleza taarifa ya Kido

Tunawapa pole majeruhi, Mwenye ez Mungu awaponye haraka ili waweze kurejea katika majukumu yao

Mwenye ez Mungu awalaze mahali Pema marehemu wote, AMEN..

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’