Bocco, Kagere wamenijenga - Miraji

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Nov 2019
Bocco, Kagere wamenijenga - Miraji

Mshambuliaji hatari wa Simba Miraji Athumani amefichua kuwa kilicho nyuma ya mabao yake ni kivuli cha nahodha, John Bocco pamoja na Meddie Kagere ambao wamekuwa wakimpa hasira ya kutafuta mafanikio.

Miraji maarufu 'Sheva' kwa sasa ametupia jumla ya mabao sita ndani ya Ligi Kuu Bara katika kikosi hicho ambacho kipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara kikikusanya pointi 25 baada ya mechi 10.

Sheva amesema kuwa anafurahi kuona anaaminiwa na benchi la ufundi na kuahidi kufunga kila anapopata nafasi.

"Nimekuwa ni mwanafunzi kwa Kagere na Bocco kutokana na uwezo wao walionao, Bocco licha ya kwamba hachezi amekuwa akinipa maneno ambayo yananiongezea hasira ya kupambana nikiwa ndani ya uwanja.

"Kwa upande wa Kagere yeye ni mchezaji wa tofauti na mfano wa kuigwa, ninaamini nitazidi kufunga kila ninapopata nafasi kutokana na ushirikiano uliopo, mashabiki wazidi kutupa sapoti kwani kazi bado ni ngumu," amesema

Straika huyo anayevaa jezi namba 21 ndani ya kikosi hicho amefunga mabao matatu kati ya sita kwa kichwa, mawili kwa mguu wa kushoto na moja kwa kulia kuonyesha ni straika mwenye uwezo wa kutumia kila kiungo chake.

Simba inafikisha jumla ya pointi 25 ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 10 kwenye Ligi Kuu Bara ikiwa imefungwa mechi moja mbele ya Mwadui FC na imelazimisha sare mbele ya Tanzania Prisons.

SportXtra

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’