Simba ni taasisi kubwa, lazima iheshimiwe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Nov 2019
Simba ni taasisi kubwa, lazima iheshimiwe

Pamoja na kuwepo kwa mgawanyiko baina ya mashabiki wa Simba kuhusu kocha wao Patrick Aussems ambaye amesimamishwa akisubiri hatma yake, yanayomtokea Aussems yana sababu

Kwa haraka haraka, kwa shabiki yeyote atashangaa kwa haya yanayoendelea baina ya uongozi wa Simba na Aussems

Pamoja na kuwa msimu huu hakufikia malengo kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, heshima aliyojijengea msimu uliopita kwa kuipeleka Simba robo fainali ya michuano hiyo, ilitosha kumfanya aendelee kuaminiwa

Aidha hata msimu huu Simba haikufanya vibaya kwenye ligi. Chini ya Aussems Simba imefungwa mchezo mmoja tu na kutoka sare mchezo mmoja. Inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia alama 25

Matokeo haya hayawezi kuwa sababu ya Aussems kuwekwa kikaangoni na mabosi wake

Tatizo liko hapa

Hivi karibuni Aussems aliondoka kwenda 'kusikojulikana' kushughulikia matatizo yake binafsi

Safari yake hiyo iliibua utata kwani Mtendaji wa Simba Senzo Mazingisa alibainisha kuwa hakuaga, alitoa taarifa akiwa uwanja wa Ndege

Hapa kuna shida, kwa nini hakuomba ruhusa? Ukiwa mwajiriwa sidhani kama Mwajiri wako atakuchekea ukiondoka eneo la kazi bila ya kuomba ruhusa hata kama ulipiga simu baada ya kuondoka

Kumekuwa na tetesi kuwa Aussems alikwenda kufanya mazungumzo na moja ya timu nchini Afrika Kusini (Polokwane City)

Mtendaji wa Simba Senzo ni mtu wa Afrika Kusini bila shaka alipatiwa taarifa zisizo na shaka na wenzake huko Afrika Kusini

Kitendo alichofanya Aussems ni kukiuka makubaliano yake na Simba

Kwani amekwenda kufanya mazungumzo na timu nyingine wakati akiwa ndani ya mkataba na Simba

Leo hii Simba ikiamua kuvunja mkataba wake hataambulia hata senti tano kwa kuwa tayari amekiuka makubaliano

Lakini pia kumekuwa na tuhuma nyingi za kinidhamu kwa wachezaji ambazo Aussems amekuwa akizifumbia macho

Kuna wachezaji ambao inaelezwa aliwapa Uhuru zaidi ya wengine. Wakati mwingine walikosa mazoezi lakini aliwapanga kwenye mechi

Hali hiyo ilichangia kushusha morali miongoni mwa wachezaji

Yeye mwenyewe pia hakuwa akifuata taratibu za ajira. Inaelezwa kuna wakati alikwenda kutembelea mbuga za Wanyawa akiiacha timu mikononi mwa kocha msaidizi kwa zaidi ya siku nne

Haya ni baadhi ya matukio ambayo pengine uongozi wa Simba ulivumilia lakini umeona wanapaswa kuchukua hatua

Ili ufanikiwe katika kazi yoyote suala la nidhamu inafaa liwe kipaumbele cha kwanza

Kama Aussems atanusurika kupoteza ajira yake, hakuna shaka atakuwa mfano kwa wengine katika kudumisha nidhamu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’