Simba yawafuatilia Chama, Mkude

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Nov 2019
Simba yawafuatilia Chama, Mkude

Ni ukweli usiopingika kuwa kiungo Clatous Chotta Chama 'Triple C' au maarufu mwamba wa Lusaka msimu huu hajafikia hata nusu ya kiwango alichokuwa nacho msimu uliopitwa wakati alipojiunga na Simba

Mwanzoni mwa msimu Simba ilimuongeza Chama mkataba wa muda mrefu baada ya kuridhishwa na kazi aliyofanya msimu uliopita

Hata hivyo tangu kuanza kwa msimu huu, Wanamsimbazi bado hawajamuona Chama yule wanaemfahamu

Kumekuwa na mijadala kumuhusu kiungo huyo ambapo wengi wanaamini baada ya kuzoea nchini, Chama ametekwa na starehe za jiji la Dar es salaam

Inaelezwa Chama ni miongoni mwa wachezaji waliomuingiza matatani kocha Patrick Aussems kwani alimpa Mzambia huyo uhuru wa kuishi anavyotaka hali iliyopelekea akasahau misingi ya kazi iliyomleta Simba

Kutokana na kuwa tayari ameshafikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu kwa matukio ya utovu wa Nidhamu, uongozi wa klabu ya Simba unamfuatilia kwa karibu kiungo huyo wa Kimataifa wa Zambia

Yeye pamoja na Jonas Mkude wamekuwa wachezaji wanaozungumzwa sana kwa kukiuka misingi ya kazi yao huku ikidaiwa kuwa Aussems alikuwa 'akiwabembeleza' kabla ya Mtendaji Mkuu Senzo Mazingisa kuingilia kati

Kama watakumbwa na matukio zaidi ya utovu wa nidhamu wanaweza kuingia kwenye matata na uongozi wa Simba ambao chini Mazingisa umeonyesha mwelekeo tofauti hasa linapokuja suala la nidhamu ya wachezaji na wafanyakazi wengine wa klabu hiyo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’