Nitaondoka kama Simba watavunja mkataba - Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Nov 2019
Nitaondoka kama Simba watavunja mkataba - Aussems

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema hana tatizo iwapo uongozi wa klabu hiyo utaamua kusitisha mkataba wake lakini mpaka sasa yeye anaendelea na majukumu yake kama kocha wa Simba

Kumekuwa na taarifa nyingi kuhusu Mbelgiji huyo ambapo baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa mchezo wa jana dhidi ya Ruvu Shooting ulikuwa wa mwisho kwake

Akizungumza baada ya mchezo huo ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, Aussems alisema taarifa nyingi zilizoripotiwa kuhusu yeye hazina ukweli wowote

Aidha Aussems amesema taarifa hizo pia zimekuwa zikiwachanganya wachezaji wake

cut

"Nyie waandishi mmekuwa mkiandika mambo mengi ambayo hayana ukweli. Wakati mwingine mmewachanganya hata wachezaji wangu"

"Nimekuwa nikipokea ofa kutoka vilabu mbalimbali kila baada ya wiki mbili lakini mpaka leo bado niko Simba"

"Nina mkataba hapa, naheshimu makubaliano yangu na klabu ya Simba. Lakini kama viongozi wa Simba wataamua kuvunja mkataba basi mimi sina tatizo," alisema Aussems

Jana baada ya mchezo mashabiki wa Simba walionyesha kumuunga mkono Aussems wakimshangilia mara baada ya mchezo kumalizika

Baadhi ya mashabiki waliusihi uongozi wa Simba usimuondoe kocha huyo kwani bado mchango wake unahitajika kwenye klabu ya Simba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
8h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’