Kukosekana kwa nahodha John Bocco kumekuwa kukiwapa hofu mashabiki wa Simba kwani Meddie Kagere anaonekana kuwa mshambuliaji pekee wa kutegemewa
Lakini Miraji Athumani amefanya vizuri kila alipopewa nafasi na ni dhahiri umefika wakati kwa benchi la ufundi kumuamini
Pamoja na kuwa hana mwendelezo mzuri wa kuanzishwa kwenye kikosi cha kwanza na kocha Patrick Aussems, Miraji ndio mshambuliaji hatari zaidi kwani amefunga na kusababisha mabao mengi ya Simba kuliko mchezaji mwingine kikosini
Mabao yake mawili aliyofunga leo kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, yamemfanya afikishe mabao sita msimu huu sasa akiwa nyuma ya Kagere kwa tofauti ya mabao mawili
Huyu ndiye Sheva ambaye ujio wake Simba haukuwa na mbwembwe nyingi lakini mpaka sasa takwimu zinambeba kuwa usajili bora uliofanywa na Simba msimu huu