Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo wanashuka katika uwanja wa Uhuru kuikabili Ruvu Shooting ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Ni mchezo ambao Simba inahitaji ushindi ili kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya Kagera Sugar kupata nafasi kuongoza kufuatia ushindi wa mchezo wao dhidi ya Lipuli Fc
Lakini pia Ruvu Shooting kupitia msemaji wao Masau Bwire wamekuwa wakitamba sana, matokeo ya ushindi yatakata 'ngebe' hizo
Kwa takwimu za michezo ya hivi karibuni, Ruvu Shooting imeshindwa kufurukuta mbele ya Simba ambapo imekuwa ikichezea vipigo vya 'mbwa koko' kili inapokutana na mabingwa hao wa nchi
Katika mchezo wa duru ya kwanza msimu uliopita Ruvu Shooting ilifumuliwa mabao 5-0 wakati msimu mmoja nyuma ilichezea kipigo cha mabao 7-1
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wamejiandaa kupata ushindi kwenye mchezo huo
Leo huenda nahodha John Bocco akarejea kikosini japo kwa dakika chache baada ya kuwa nje kwa miezi mitatu
Kikosi cha Simba kiko kamili baada ya nyota wake wote waliokuwa na majukumu ya Kimataifa kurejea
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi jioni