Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kesho wanahitaji ushindi ili kuweza kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya leo kushushwa nafasi ya pili na Kagera Sugar
Kagera Sugar imeifunga Lipuli Fc mabao 2-1 hivyo kufikisha alama 23, alama moja zaidi ya Simba yenye alama 22
Kagera Sugar imecheza mechi mbili zaidi ya Simba ambayo kesho itacheza na Ruvu Shooting
Uongozi wa Kagera Sugar unaweza kuwa wa muda mfupi kwani ushindi au hata matokeo ya sare kwa Simba kesho, yatatosha kuwarudisha kileleni

ADVERTISE HERE