Simba yaahidi kurejea na ubingwa kombe la Mapinduzi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Jan 2018
Simba yaahidi kurejea na ubingwa kombe la Mapinduzi
Kikosi cha Simba, kimewasili mapema leo Kisiwani Zanzibar na kufikia hoteli ya nyota tano iliyo nje kidogo ya mji

Timu hiyo ambayo haikutaka kuweka wazi jina la hoteli, imesafiri na wachezaji 24 pamoja na viongozi 6, ambao kama watafanya vizuri wataendelea kukaa kisiwani humo mpaka mashindano yatakapofikia kikomo Januari 13, siku itakapochezwa mechi ya fainali.

Kocha wa Simba Masoud Djuma amesema, kikosi chao kimewasili salama na wanachofikilia wakati huu ni mechi yao ya kwanza kesho dhidi ya Mwenge itakayochezwa jioni kwenye Uwanja wa Amaan.

"Hatukuwa na muda wa kutosha kujiandaa, tumetoka kucheza mechi ya ligi Mtwara hatuja pumzika, tumepitiliza kuja huku na kesho tunacheza, hata mazoezi mazuri ya maandalizi yetu hatujafanya," amesema Djuma.

Kocha huyo ambaye amerithi mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu, Mcameroon Joseph Omog amesema, pamoja na changamoto hizo, watahakikisha wanafanya viziri kwenye mashindano haya.

Azam FC ndiyo mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi ambalo walilitwaa mikononi mwa Simba mechi ya fainali kwa ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Himid Mao.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’