Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kimewasili usiku wa kuamkia leo kutoka Tunisia ambako kilicheza mechi ya kusaka tiketi ya michuano ya Afcon 2021 na kufungwa mabao 2-1
Nyota watano wa Simba waliokuwa kwenye kikosi hicho sasa wanaongeza nguvu kwenye kikosi cha Simba kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa Jumapili
Aidha Sharaff Shiboub, Clatous Chama na Meddie Kagere nao wanatarajiwa kuanza kuripoti kambini kesho Ijumaa baada ya kumaliza majukumu ya timu za mataifa yao
Wakati wa kalenda ya Kimataifa Simba iliwakosa wachezaji wake 10 ambao waliitwa timu za Taifa
Hata hivyo Simba imepata pigo kwa beki wake kiraka Erasto Nyoni kuumia kwenye mchezo kati ya Tanzania dhidi ya Guinea ya Ikweta ambao ulipigwa jijini Dar es salaam
Nyoni hakusafiri na Stars kwenda Tunisia