Bado suala la kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems halijapoa, inaelezwa leo atakuwa na kikao na mabosi wa Simba akitakiwa atoe maelezo kwa nini aliondoka bila ya kuomba ruhusa
Lakini suala jingine inaelezwa tayari uongozi wa Simba umeshafikia uamuzi wa kuachana na Aussems ni suala la muda tu Mbelgiji huyo atakabidhiwa barua ya kuvunjwa mkataba wake
Taarifa za ndani zimebainisha kuwa Simba imewasiliana na Pierre Lechantre aliyekuwa kocha wake kabla ya kumuajiri Aussems
Lakini pia zipo tetesi kuwa Simba inamuwania Florent Ibenge, kocha wa AS Vita
Katika mpango wake wa miaka mitano, Simba imedhamiria kupiga hatua hasa kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika, CV za makocha hao ni ishara tosha ya mwelekeo ambao SImba inataka kuchukua
Lechantre alichukua mikoba ya kuinoa Simba kutoka kwa Joseph Omog ambapo akishirikiana na Masudi Djuma, waliiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa ligi kuu
Lechantre ana CV kubwa kwenye soka la Afrika, mwaka 2000 aliongoza timu ya Taifa ya Cameroon kutwaa taji la Afcon
Inaelezwa kuondoka kwake mwanzoni kulitokana mahitaji makubwa ya mshahara ambao aliuhitaji wakati ule ambao ulikuwa zaidi ya bajeti ambayo Simba ilikuwa imetenga kwa ajili ya kocha