Singida United yamtaka Ndemla

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Nov 2019
Singida United yamtaka Ndemla

Kocha Mkuu wa Singida United Nsanzurwimo Ramadhani ameonyesha nia kumtaka kwa mkopo kiungo wa Simba Said Khamis Ndemla ambaye amekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa nchi

Singida United imekuwa na wakati mgumu msimu huu, inaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi, ikiwa imejikusanyia alama nne tu

Nsanzurwimo amesema wamedhamiria kuhakikisha wanaibakisha timu hiyo ligi kuu hivyo watatumia usajili wa dirisha dogo kusajili nyota wenye uwezo

Hata hivyo changamoto za kiuchumi zilizoikumba timu hiyo huenda zikawafanya washindwe kuipata huduma ya Ndemla kutokana na masharti yaliyowekwa na Simba kwa timu zinazowataka wachezaji wake kwa mkopo

Hivi karibuni Mtendaji wa Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa alisema timu yoyote inayomtaka mchezaji wa Simba kwa mkopo lazima ithibitishe kuwa na uwezo wa kumlipa mshahara wake anaolipwa Simba kwa muda wote atakaoichezea timu hiyo

Alisisitiza Simba haitakuwa tayari kuingia gharama ya kulipa mishahara ya wachezaji ambao wanazichezea timu nyingine kwa mkopo

Klabu ya KMC nayo inamuwania kwa mkopo winga Rashid Juma

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’