Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems anatarajiwa kurejea nchini leo, uongozi wa Simba umebainisha
Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema Mbelgiji huyo aliomba ruhusa ya siku tatu kwenda kushughulikia masuala binafsi
Aidha mapema jana Aussems mwenyewe alithibitisha kuwa atarejea nchini leo kuendelea kuiandaa timu kuelekea mchezo dhidi ya Ruvu Shooting
Kumekuwa na tetesi nyingi kumuhusu bosi huyo ambaye msimu uliopita aliiongoza Simba kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa pamoja na kutetea ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa pili mfululizo
Hata hivyo uongozi wa Simba umesisitiza kuwa Aussems bado ni mwajiriwa wa Simba, yanayozungumzwa huko mtaani yabaki kuwa tetesi tu
ADVERTISE HERE