TAARIFA
Kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ndugu Swedy Mkwabi, Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Simba Sports Club Limited imemteua Ndugu Mwina Mohammed Kaduguda kuwa Kaimu Mwenyekiti wa klabu ya Simba. Uteuzi huu umeanza terehe 10 Novemba 2019
Tarehe ya uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa klabu ya Simba itatangazwa na Bodi ya Wakurugenzi hapo baadae
Vilevile Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Simba Sports Club Limited imemteua Salim Abdallah Muhene kuwa Makamu Mwenyekiti. Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Novemba 2019
Teuzi hizo zimefanyika kwa mujibu wa Mamlaka ya Bodi chini ya ibara ya 50 ya Katiba ya klabu ya Simba
ADVERTISE HERE