Aussems atuliza hofu Simba, atarejea Jumatano

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Nov 2019
Aussems atuliza hofu Simba, atarejea Jumatano

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amethibitisha kuwa ni kweli hayuko nchini akishughulikia masuala binfasi

Amesema kesho Jumatano atarajea kuendelea kukiandaa kikosi chake kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting

Mchezo huo utapigwa Jumapili Novemba 24 kwenye uwanja wa Uhuru

"Nimelazimika kuondoka kwa siku mbili kushughulikia masuala binafsi. Nitakuwepo kesho (Jumatano) kuiandaa timu kwa ajili ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting. Malengo yetu ni kushinda mchezo huo," amesema Aussems

Taarifa za Aussems kuondoka nchini zilianza kusambaa jana baada ya Mbelgiji huyo kukosekana kwenye mazoezi ya asubuhi

Kukosekana kwake kuliongeza sintofahamu juu ya hatma yake kwani zipo tetesi kuwa kuna jambo linaendelea baina yake na uongozi wa Simba kuhusu hatma yake

Lakini wakati huohuo watu wake wa karibu wanadai kuwa nae ameamua kuweka sawa mipango yake ikitokea ametimuliwa Simba

Nkana Fc na AS Vita zinatajwa kuvutiwa na Aussems ambaye msimu uliopita aliifikisha Simba robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’