Aussems awashangaa wanaotaka atimuliwe Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Nov 2019
Aussems awashangaa wanaotaka atimuliwe Simba

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ameeleza kushangazwa na baadhi ya mashabiki kukosa imani nae licha ya kuwa timu haina matokeo mabaya

Mbelgiji huyo amesema pamoja na changamoto kadhaa ambazo kikosi chake kinapitia lakini anaamini ana kikosi imara ambacho kitafanya vizuri msimu huu

"Lazima ukutane na changamoto katika mahala popote ambapo unafanya kazi na hilo nadhani ndio lipo wakati huu, lakini kama haitoshi kila kocha anaajiriwa ili afukuzwe kwa maana hiyo sina hofu yoyote na ninaendelea na majukumu yangu," Aussems amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

"Hata kama itatokea kutimuliwa, sitakuwa wa kwanza kwa vile katika soka hakuna kocha wa kudumu, ila bado naamini Simba haina sababu ya kuwa na presha kwa sasa, tuna kikosi imara nasi tunatekeleza majukumu yetu kwa ajili ya kuwapa furaha mashabiki"

Presha dhidi ya Aussems ilianza baada ya Simba kupoteza mchezo dhidi ya Mwadui Fc kwa kufungwa bao 1-0 mkoani Shinyanga

Kipigo hicho kilikumbusha machungu ya kuondoshwa hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo

Matokeo ya suluhu dhidi ya Tanzania Prisons na kipigo dhidi ya KMC kwenye mchezo wa kirafiki juzi, kimeongeza minon'gono kumuhusu kocha huyo ambaye msimu uliopita aliifikisha Simba robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa

Aussems anaendelea kukiandaa kikosi chake kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa Jumapili Novemba 24 kwenye uwanja wa Uhuru

Ni mchezo ambao Simba inahitaji kushinda ili kurudisha hali ya utulivu kwa mashabiki wake kwani matokeo tofauti na ushindi yanaweza kumuweka kwenye wakati mgumu Aussems

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’