Timu ambazo zinawahitaji nyota wa Simba kwa mkopo zimeaswa kuwa ni lazima ziwe na uwezo wa kuwalipa wachezaji hao mishahara
Mtendaji wa Simba Senzo Mazingisa amesema timu hiyo imekuwa ikiingia gharama kuwalipa mishahara wachezaji ambao wametolewa kwa mkopo
Amesema kuanzia sasa hawatakuwa tayari kuwalipa wachezaji ambao wanazitumikia timu nyingine kwa mkopo, litakuwa jukumu la timu wanazocheza
Hivyo moja ya masharti yao kwa timu zinazowataka lazima ziwe na uwezo wa kuwalipa mishahara
"Wapo wachezaji tunakusudia kuwatoa kwa mkopo kwenda timu nyingine ili tuweze kufanya usajili dirisha dogo. Lakini timu ambazo zitawachukua wachezaji hawa lazima ziwe na uwezo wa kuwalipa," amesema
"Klabu nyingi ambazo zimekuwa zikihitaji wachezaji wetu kwa mkopo, zinashindwa kuwalipa mishahara. Tunahitaji timu hizo ziwe na uwezo wa kuwalipa"
Simba imedhamiria kuboresho kikosi chake dirisha dogo ili kuhakikisha inatetea ubingwa kwa msimu wa tatu ili kujihakikishia tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao