Senzo ataja Ligi ya Mabingwa kuwa kipaumbele Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
17 Nov 2019
Senzo ataja Ligi ya Mabingwa kuwa kipaumbele Simba

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa raia wa Afrika Kusini amefichua kuwa mikakati yake ni kuona timu hiyo inacheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika kila msimu.

Mazingisa ambaye amefanya kazi na baadhi ya klabu kubwa za nchini Afrika Kusini ikiwemo Platnumz Stars iliyowahi kushiriki ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama PSL akiwa kama Meneja Mkuu.

Mbali ya Platnumz, Mazingisa aliiongoza Orlando Pirates kwa mafanikio katika kipindi cha mwaka 2011 hadi 2013

Mazingisa amesema mikakati aliyonayo ni kuiona Simba inacheza hatua makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kila msimu kwa lengo la kuongeza kipato cha timu hiyo

"Mkakati wangu ni kwamba nataka kuona Simba chini yangu inacheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kila msimu hilo ndiyo jambo kubwa ambalo naliona kwa sasa," Mazingiza alinukuliwa na gazeti la SportXtra

"Unajua hii michuano kufika katika hatua ya makundi inakuwa ni jambo zuri kwa sababu kipato cha timu kinakuwa kinaongezeka, tumepoteza msimu huu ni sawa na kusema ni hasara kwetu lakini tunapoendea nataka kuona kila msimu tunacheza makundi"

Baada ya kucheza hatua ya robo fainali msimu uliopita, msimu huu mambo hayakuwa mazuri kwani mabingwa hao wa Tanzania Bara waliondoshwa hatua ya awali

Ili kujihakikishia kushiriki michuano hiyo msimu ujao, Simba inapaswa kutetea ubingwa wake walioutwaa kwa misimu miwili mfululizo

Mpaka sasa hesabu ziko salama kwani mabingwa hao wanaongoza ligi baada ya kushuka dimbani mara tisa, wamejikusanyia alama 22

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →