Mchezo wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya KMC, umemalizika kwa KMC kuondoka na ushindi wa mabao 2-1
Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi, ulishuhudiwa na idadi kubwa ya mashabiki ambao leo walipata fursa ya kuingia bila kiingilio
Mabao yote yalifungwa kwenye kipindi cha pili ambapo ya KMC yalifungwa na Kenny Ally Mwambungu wakati bao la kufutia machozi kwa upande wa Simba lilifungwa na Ibrahim Ajib kwa mkwaju wa penati wakati mchezo huo ukielekea ukingoni

Leo Simba imecheza chini ya kiwango, haikuwa katika ubora wake uliozoeleka
Pamoja na kuwakosa nyota walio timu za Taifa, wachezaji waliobaki walipaswa kufanya vizuri kwenye mchezo huu kwani ilikuwa nafasi kwa baadhi yao kumshawishi kocha Patrick Aussems
Bila shaka Aussems atakuwa ameona mapungufu ya kikosi chake, maboresho yatahitajika kabla ya mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa Novemba 24