Ukizungumzia wachezaji wanaofanya vizuri katika soka la Tanzania wakati huu, hutakosa kutaja jina la Bakari Nondo Mwamnyeto beki wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' na timu ya Coastal Union
Akiwa na umri wa miaka 22 Mwamnyeto tayari ameoneka kuwa mbadala sahihi wa wakongwe Erasto Nyoni na Kelvin Yondani katika timu ya Taifa
Mwamnyeto anafanya vizuri sana timu ya Taifa, jana katika mchezo dhidi ya Guinea ya Ikweta alionyesha kiwango kizuri
Inaelezwa tayari uongozi wa Simba umeanza mchakato wa kumnasa beki huyo wakati wa usajili wa dirisha dogo litakalofunguliwa Disemba 16
Simba inatarajiwa kufanya maboresho ya kikosi chake dirisha dogo lakini usajili wa Mwamnyeto utakuwa mpango wa muda mrefu
Beki huyo anatajwa kuja kuchukua nafasi ya Paschal Wawa ambaye msimu ujao huenda asiwe sehemu ya kikosi cha Simba