Stars yaichapa Guinea ya Ikweta 2-1

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Nov 2019
Stars yaichapa Guinea ya Ikweta 2-1

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imeanza vyema kampeni ya kusaka tiketi ya fainali za Afcon 2021 baada ya kuichapa Guinea ya Ikweta mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa

Guinea ya Ikweta ilitangulia kupata bao la kuongoza kupitia kwa mkongwe Pedro Obiang anayechezea Sassuolo inayoshiriki ligi kuu ya Italia, Serie A

Akiwa nje ya 18, Obiang alitandika mkwaju mkali ambao ulimshinda mlinda lango wa Stars Juma Kaseja

Stars iliyotawala mchezo huo kwa muda mwingi ilikosa bahati ya kutumbukiza mpira kimiani kwenye kipindi cha kwanza licha ya kutengeneza nafasi nyingi

Haikuwa siku nzuri kwa nahodha Mbwana Samatta ambaye majaribio yake yaliokolewa na mlinda lango wa Guinea ya Ikweta

Kipindi cha pili kocha wa Stars Etienne Ndayiragije alibadili mbinu za kimchezo akimuingiza mshambuliaji Ditram Nchimbi nafasi ya Hassan Kessy

Alibadili mfumo wa uchezaji kutoka 4-3-3 na kuwa 4-4-2 ambapo Erasto Nyoni aliyeanza mchezo kama kiungo mkabaji alirudi nyuma kucheza sambamba na Bakari Mwamnyeto wakati Kelvin Yondani akihamia upande wa beki wa kulia

Mabadiliko hayo yaliinufaisha Stars kwani iliendelea kutawala mchezo

Alikuwa ni Saimon Msuva aliyeisawazishia Stars kwenye dakika ya 68 baada kuwahi krosi iliyochongwa na Hassan Dilunga

Wakati mchezo huo ukielekea ukiongoni, Salum Abubakar aliihakikishia Stars alama tatu muhimu baada ya mkwaju wake aliopiga nje ya 18 kuzama nyavuni ukimshinda mlinda lango wa Guinea ya Ikweta

Ushindi huo unaiweka Stars kileleni mwa kundi J ikiwa na alama tatu na mabao mawili

Baadae Tunisia itachuana na Libya

Stars inatarajiwa kusafiri kwenda nchini Libya tayari kwa mchezo wa pili utakaopigwa Novemba 19

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’