Timu ya Taifa ya Zambia jana ilikwama mbele ya mabingwa wa Afrika Algeria baada ya kukubali kipigo cha mabao 5-0 katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za Afcon 2021 zitakazofanyika nchini Cameroon
Kikosi cha Zambia kilichoanza mchezo huo uliopigwa nchini Algeria, kilimjumuisha nyota wa Simba, fundi Clatous Chotta Chama 'CCC'
Zambia iliruhusu mabao hayo katika dakika 30 za mwisho
Wakati Chama akianza vibaya michuano hiyo, hali ilikuwa hivyo kwa Meddie Kagere na kikosi cha Rwanda
Rwanda ilifungwa mabao 2-0 na Msumbiji katika mchezo ambao ulijaa malalamiko ya upendeleo kwa wenyeji Msumbiji
Rwanda waliruhusu mabao yote mawili kwenye kipindi cha kwanza huku bao la kwanza likifungwa na Msumbiji kupitia mkwaju wa penati ambao ulilalamikiwa na wachezaji wa Rwanda
Leo Tanzania itakuwa uwanja wa Taifa kuumana na Guinea ya Ikweta