Kibadeni, Mwaisabula wachambua kinachomsumbua Chama

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Nov 2019
Kibadeni, Mwaisabula wachambua kinachomsumbua Chama

Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah "King" Kibadeni pamoja na mdau na nguli wa soka nchini, Kenny Mwaisabula wametofautiana kimtazamo katika maoni yao kuhusu madai ya kuporomoka kiwango kwa kiungo wa Wekundu wa Msimbazi, Mzambia Clatous Chama.

Chama ameingia katika mjadala mzito kupitia mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kinachotafuna kiwango chake kwa sasa ukilinganisha na ubora wa hali ya juu aliokuwa nao msimu uliopita.

Hata hivyo, wakati Kibadeni akisema kinachomtesa zaidi Chama ni kutokana na ushindani mkubwa wa namba uliopo Simba kwa sasa, Mwaisabula yeye amefunguka kuwa starehe nyingi huenda kikawa chanzo cha kiungo huyo raia wa Zambia kuporomoka kisoka.

"Pale Simba kwa sasa kuna ushindani mkubwa katika nafasi ya kiungo anayocheza Chama, kuna wachezaji kama Kahata [Francis] ambaye anakuja juu kwa sasa na pia Ajibu [Ibrahimu] na wengine, hivyo anajikuta hapati namba mara kwa mara, jambo ambalo inakuwa vigumu kuonekana kuwa katika kiwango bora," alisema Kibadeni.

Lakini Mwaisabula alisema Chama amekuwa miongoni mwa nyota wanaoelekea kuporomoka kwa kasi kiwango chake ukilinganisha na wakati anatua Simba akitokea Power Dynamos ya Zambia.

"Inaonekana starehe zinamgharimu Chama na sasa hana tena ule ubora wake dimbani. Huyu si yule Chama ninayemfahamu, si yule wa Simba wa mwaka jana, wachezaji wengi wa nje wakija Tanzania hawamalizi mwaka mmoja wanapotea dimbani, wanaendekeza starehe zaidi kuliko kazi," alisema.

Mbali na Ajibu na Kahata, lakini pia nafasi hiyo ya Chama anaweza kuicheza vizuri Mtanzania Hassan Dilunga pamoja Sharaf Eldin Shiboub aliyesajiliwa msimu huu akitokea kwao Sudan, ambaye pia ameanza kunyoshewa kidole kuwa uwezo wake umeanza kushuka mapema

Nipashe

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’