Stars kuanza kampeni ya kusaka tiketi Afcon 2021

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Nov 2019
Stars kuanza kampeni ya kusaka tiketi Afcon 2021

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo inashuka uwanja wa Taifa kuikabili Guinea ya Ikweta katika mchezo wa kwanza wa kusaka nafasi ya kutinga fainali za Afcon 2021 ambazo zitafanyika nchini Cameroon

Mchezo huo wa kwanza kundi J utapigwa saa moja usiku

Hii ni nafasi kwa Stars kuanza vyema kampeni ya kwenda Cameroon

Katika michuano iliyopita ambayo ilifanyika Misri, Stars ilishiriki kwa mara ya pili katika historia yake

Ilianza kampeni yake kwa kucheza na Lesotho mchezo ambao ulipigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi na kumalizika kwa sare ya bao 1-1

Kocha Mkuu wa Stars Etienne Ndayiragije amesema hawako tayari kurudia makosa ya kukosa ushindi katika mchezo huo wa kwanza

Mbwana Samatta, nahodha wa Stars amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa ili kuwaunga mkono katika mchezo huo

Guinea ya Ikweta iliwasili nchini juzi, jana jioni ikafanya mazoezi katika uwanja wa Taifa

Timu hiyo imesheheni nyota wengi wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya hasa Hispania ambapo nyota wake wengi wanacheza timu za madaraja ya chini

Wakati Stars ikichuana na Guinea ya Ikweta, mchezo mwingine wa kundi J utazihusisha Tunisia na Libya

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
29m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’