Simba kuhamia Bunju kabla ya Disemba 08

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Nov 2019
Simba kuhamia Bunju kabla ya Disemba 08

Uongozi wa Simba umesema kuwa, kabla ya kufanyika kwa mkutano Mkuu, watakuwa tayari wameuzindua uwanja wao uliopo Bunju jijini Dar es Salaam.

Simba chini ya mwekezaji wake, Mohammed Dewji ‘Mo’, ulianza kujenga uwanja wao wa mazoezi ambapo awali ulitarajiwa kumalizika Februari, mwaka huu, lakini changamoto zilizojitokeza zikakwamisha ujenzi huo ambao sasa imetangazwa utakuwa sawa Desemba, mwaka huu.

Katibu wa Simba, Anold Kashembe, amesema kikubwa kinachokwamisha kukamilika kwa uwanja huo ni kutokana na mvua zisizoeleweka kuendelea kunyesha mara kwa mara.

"Kuna mvua ambayo imenyesha hapa kati ndiyo imetibua hasa katika ule uwanja wa nyasi bandia ambapo ule udongo umevurugika, lakini upande wa nyasi asilia mambo yanakwenda vizuri," amesema

"Kutokana na hilo, tarehe 7 ya mwezi ujao, kabla ya Mkutano Mkuu haujafanyika, tunatarajia kuuzindua rasmi uwanja wetu"

"Unajua tumekuwa tukitumia gharama nyingi sana sehemu ambayo tumekuwa tukienda kufanya mazoezi, hivyo tumeamua kuitengeneza pitch (sehemu ya kuchezea) haraka, kisha masuala ya hosteli na mengine yatafuata"

Desemba 8, mwaka huu, Klabu ya Simba inatarajiwa kufanya mkutano mkuu ambapo siku moja kabla ya mkutano huo, ndipo watauzindua uwanja wao

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
7h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
13h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
16h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’