Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema katika mpango wa kuhakikisha bidhaa za klabu hiyo zinainufaisha timu, bidhaa zote zitapatikana katika Matawi kote nchini
Mazingisa alisema Simba inaweza kuitumia utaratibu wa kuanza kuthibitisha wanachama na matawi yaliyopo kujiingizia kipato na kuchangia kukua kwa uchumi wa Tanzania.
"Najua katika hili tunaweza kufanikiwa. Kama ni shabiki wa Simba, hutakiwi kupata bidhaa zetu kwa njia ya mkato, tutakuwa na utaratibu ambao utawafanya kupata bidhaa mbalimbali za klabu kupitia matawi, ni njia nyepesi," Senzo amenukuliwa na Mwanaspoti
"Kwa kushirikiana na wanachama ina maana mashabiki wa Simba, wataachana na mambo ya kununua bidhaa feki hivyo klabu itajiingizia kipato kwa mfano, wanachama 1000 wamehusika kuchukua bidhaa, unadhani ni kiasi gani kitaingia? Sasa tunatakiwa kufika huko."
Ili kufikia malengo ya kuwa klabu kubwa barani Afrika, Senzo amesema wanapaswa kujiimarsiha kiuchumi na hilo ndilo lililomleta nchini ili kuwa sehemu ya ukuaji huo.