Mshambuliaji hatari wa Simba Meddie Kagere leo ataiongoza timu ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi' kuikabili Msumbuji kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya michuano ya Afcon 2021 ambayo itafanyika Cameroon
Kagere ataungana na 'swahiba' wake Jacques Tuyisenge katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi kuelekea safari ya Cameroon
Jana nyota mwingine wa Simba Sharaff Elden Shiboub aliibeba Sudan katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Sao Tome akifunga moja ya mabao hayo
Lakini pia kiungo Clatous Chama yuko nchini Algeria na kikosi cha Zambia wakitarajiwa kuwakabili mabingwa watetezi Algeria baadae leo
Mzamiru, Tshabalala, Gadiel, Nyoni, Dilunga na Miraji wao watakuwa 'mzigoni' kesho wakati Taifa Stars itakapoikaribisha Equatorial Guinea uwanja wa Taifa
Nyota tisa wa Simba wanakabiliwa na majukumu ya timu za Taifa wiki hii