Kaseja afunguka baada ya kauli ya Mgunda, asema Stars ni ya wote

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Nov 2019
Kaseja afunguka baada ya kauli ya Mgunda, asema Stars ni ya wote

Wakati mjadala wa kuachwa kipa wa Simba, Aishi Manula katika kikosi cha Taifa Stars ukizidi kupamba moto, huku Juma Mgunda akiandamwa kwa kauli yake dhidi ya mlinda mlango huyo, Juma Kaseja amesema timu hiyo ni ya Watanzania wote na hawana budi kuungana pamoja Uwanja wa Taifa kesho

Mashabiki wa soka nchini wamekuwa wakilalamika kwa kitendo cha Manula kutoitwa Stars, huku Mgunda akilaumiwa kwa kauli yake aliyoitoa alipoulizwa kwa nini kipa huyo hakujumushwa katika kikosi hicho.

Kikosi cha Stars kilichopo kambini kujiandaa na mechi dhidi ya Equatoria Guinea kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2021, baada ya kutangazwa, Mgunda aliulizwa kwa nini Manula hakujumuishwa katika timu hiyo na kujibu "hawaangalii sura", kauli ambayo imezua mjadala mzito kwa mashabiki, mitandao ya kijamii na hata kwa baadhi ya vyombo vya habari.

Hata hivyo, Mgunda ametolea ufafanuzi vizuri akieleza kuwa hakuwa na lengo baya kwa Manula na kwamba alinukuliwa vibaya kwa kuchukuliwa sehemu fupi ya mazungumzo yake kwani alikuwa akiimaanisha wameita kikosi hicho kulingana na mahitaji ya sasa na kwamba bado wanaheshimu mchango wa kipa huyo na kwamba huu si mwisho kwake kukitumikia Stars.

Lakini Kaseja akizungumzia timu hiyo alisema Taifa Stars ni ya wachezaji wote walioitwa na wasiotwa kuitumikia kwa sasa, lakini pia ni ya Watanzania wote, na kwamba huu ni wakati wakuungana pamoja kwenda kuisapoti uwanjani.

"Timu hii ni ya Watanzania wote, waliopo ndani ya kikosi na ambao hawakuitwa, cha muhimu kwa sasa ni kushirikiana kuelekea katika mechi yetu dhidi ya Equatorial Guinea," alisema

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’