Nahodha wa Timu ya Taifa 'Taifa Stars' Mbwana Samatta jana aliingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kufuzu AFCON 2021 dhidi ya Equatorial Guinea ambao utapigwa keshokutwa Ijumaa Novemba 15 Uwanja wa Taifa.
Samatta anayecheza KRC Genk ya Belgium anatarajia kuiongoza Taifa Stars katika mchezo huo dhidi ya Equatorial Guinea na mchezo utakaofuata siku 4 baadaye dhidi ya Libya utakaochezwa ugenini.
Wachezaji wengine wanaocheza nje ya Tanzania ambao tayari wameingia kambini ni pamoja Saimon Msuva (Difaa, Morocco), Farid Mussa anayecheza Tenerife ya Hispania, David Kisu(Gor Mahia,Kenya),Ramadhan Kessy (Nkana,Zambia) na Eliuter Mpepo (Buildcon,Zambia)
Taifa Stars inajifua kwenye Uwanja wa Taifa ikipiga Kambi katika Hoteli ya Blue Saphire,barabara ya Pugu jijini Dar es salaam
Mchezo dhidi ya Equatorial Guinea utachezwa saa 1 usiku Uwanja wa Taifa Ijumaa Novemba 15.
Kiingilio kwenye mchezo huo ni shilingi 3,000 mzunguko,5,000 VIP B na C