Mwishoni mwa wiki hii dirisha dogo la usajili litafunguliwa kuzipa nafasi timu za ligi kuu na ligi daraja la kwanza kuimarisha vikosi vyao
Mabingwa watetezi Simba hawatarajiwi kuwa 'busy' sana kwenye dirisha hili kutokana na ubora wa kikosi chao
Hata hivyo kulingana sera alizokuja nazo CEO mpya, Senzo Mazingisa, ni wazi michakato ya usajili itafanyika
Mazingisa ametaka kuona wachezaji wote wanakuwa na mchango kwenye timu
Wale ambao hawana nafasi, bosi huyo amemuagiza Aussems ampe ripoti kwa nini wachezaji hao hawachezi
Kwa wale ambao hawaonekani kuingia katika mipango ya Mwalimu, wanaweza kuachwa au kutolewa kwa mkopo
HATMA YA WABRAZIL
Moja ya mambo ambayo yanaelezwa kumshangaza Mazingiza ni usajili wa nyota watatu kutoka Brazil, Tairone Da Silva, Wilker na Fraga
Bosi huyo alisema wanaweza kuwapata wachezaji wenye uwezo sawa au zaidi ya Wabrazil hao ukanda huu huu wa Afrika Mashariki tena kwa gharama nafuu zaidi
Hivyo ni dhahiri, hatma yao iko mikononi mwa Aussems
Tairone na Fraga wamekuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Aussems
Fraga amekuwa na mchango zaidi kati yao lakini Wilker anaweza kuwa hatarini kwa kuwa mchango wake haujaonekana mpaka sasa
Amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara
Katika moja ya mahojiano yake, Aussems alisema mchezaji huyo hayuko 'fit' kuhimili mikiki-mikiki ya ligi kuu