Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa wiki hii (Novemba 15) ambapo timu za Ligi Kuu na Ligi daraja la kwanza zitakuwa na nafasi ya kuimarisha vikosi vyao
Uongozi wa Simba umepanga kufanya maboresho ya kikosi chake ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa walioutwaa kwa misimu miwili mfululizo
Aidha baadhi ya nyota ambao wamekosa nafasi huenda wakatolewa kwa mkopo
Miongoni mwa wachezaji hao ni winga kinda Rashid Juma ambaye msimu huu hajapata kabisa nafasi ya kucheza kwenye ligi
KMC imeonyesha nia ya kumtaka Juma kwa mkopo, upo uwezekano mkubwa kuwa ataruhusiwa kujiunga na timu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu
Yusuf Mlipili ni nyota mwingine ambaye anaweza kutolewa kwa mkopo
Mlipili hana nafasi kwenye kikosi cha kocha Patrick Aussems