Simba yarejea mazoezi kuiwinda Ruvu Shooting

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Nov 2019
Simba yarejea mazoezi kuiwinda Ruvu Shooting

Baada ya mapumziko ya siku tatu, kikosi cha Simba kimerejea mazoezi leo kuendelea na maandalizi ya mchezo unaofuata wa ligi kuu ambao ni dhidi ya Ruvu Shooting

Mchezo huo utapigwa Novemba 24 katika uwanja wa Uhuru

Hata hivyo Simba inawakosa wachezaji wake 10 ambao wanakabiliwa na majukumu ya timu za Taifa

Ili kuhakikisha program za mazoezi zinakamilika kama zilivyopangwa, Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema nyota wengine wa timu ya vijana watajumuishwa kikosi cha kwanza

Baada ya kupunguzwa kasi mchezo uliopita, vinara hao wa ligi kuu wamedhamiria kurejea kivingine mechi dhidi ya Ruvu Shooting

Simba inasimama kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 22 baada ya kushuka dimbani mara tisa

Imefunga mabao mengi zaidi kuliko timu nyingine (16) na imefungwa mabao machache zaidi (3)

Kinara wa kuzifumania nyavu ni Meddie Kagere aliyetupia mabao manane mpaka sasa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
13h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
16h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’